A Polite KiSwahili Rant and A bit of Eric Wainaina

February 18, 2014

Kuna mambo machache ambayo ningependa kusema. Iwapo mambo haya huenda yakawa si muhimu kwenye maisha ya mwanadamu kama mimi au wewe, ni vyema kuyazingatia haswa ikiwa unauamini ubinadamu na haki. Hivyo basi naomba mniwie radhi iwapo huenda jambo nitakalolisema likakwaza fikra na hisia za uzalendo wako. Huenda mkakosa kuyasoma au kuyaelewa kwa sababu Kiswahili changu si chema au sizungumzi kwa lafudhi unayoifahamu wewe.

Kwa miaka mingi nimegundua kwamba Kenya ni kati ya nchi chache ulimwenguni ambapo nimeona ishara zaidi za tabia za kutojali. Tabia ambazo nimeshuhudia si nadra kwenye mitandao ya uhusiano usio wa usoni kama vile utani tunaouona baada ya vurugu za kijinsia kwenye mitandao kama hii. Kwa mfano iwapo wacheshi wa humu nchini wataendelea kuwafedhehesha wanawake, maskini, ‘mashoga’, WaIslaamu, waathirika wa vurugu za baada ya uchaguzi, wanaofanya biashara ya ngono, waathirika wa ubakaji na wengi walio pembezoni swali langu basi ni, “Je, twacheka nini?” na “Twamcheka nani?”

Maswali haya mawili mtawalia si ya uzalendo bali ni maswali yanayoguzia jinsi tunavyotaka kuishi ulimwenguni kama binadamu wa kuheshimika wanaouhoji upendeleo na hadhi zinazowapa wao neema kwenye jamii. Huenda ikawa maneno ninayoyasema si ya Kiungu bali ni mambo machache ambayo yaiumiza roho yangu kwenye nchi iliyo kama meli kwenye makeke. 

Mash’allah!

 

Just a bit of Eric even for the unpatriotic me: http://www.youtube.com/watch?v=Dh3oKHJ7KZQ&list=RDVn6Mg5yjoY8

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *